Kartra

Msuva Aitamani Simba SC Robo Fainali CAF

WINGAwa Klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco, Simon Msuva amesema kuwa anatamani kukutana na Simba katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani anaamini itakuwa mechi nzuri katika msimu huu wa ligi hiyo.

Msuva katika msimu huu wa ligi hiyo akiwa na Wydad Casablanca amefanikiwa kufunga mabao miwili katika michezo minne aliyocheza mpaka sasa.

 

Amesema ubora wa Simba na Wydad anaamini wakikutana katika mchezo wa robo fainali wa ligi hiyo utakuwa mchezo mzuri huku akisema kuwa ubora wa Simba wanapokuwa katika Uwanja wa Mkapa hautakuwa kikwazo kwao kuizua Simba.

“Natamani kuona tunakutana na Simba katika hatua ya robo fainali kwani utakuwa mchezo mzuri sana katika ligi ya mabingwa msimu huu kwani itazikutanisha timu bora ambazo zote zinafanya vizuri kwa sasa.

 

“Najua kuwa Simba wanapokuwa katika Uwanja wao wa nyumbani kwa Mkapa huwa hawakubali kupoteza mchezo lakini sisi Wydad tumezoea kucheza michezo mingi na tumezoea hivyo haitakuwa kikwazo kwetu kushindwa kuizuia Simba,” alisema winga huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam


Toa comment