The House of Favourite Newspapers

Msuva Akataa Mshahara wa Mil 9 Kwa Mwezi

0
Mchezaji wa Yanga, Simon Msuva.

OFA ya Simon Msuva kwenda Morocco imekamilika na klabu ya Difaa El Jajida kutoka nchini humo iko tayari kumwaga dola 4,000 (takriban Sh milioni 9) kumlipa mshahara kila mwezi. Lakini taarifa zinaeleza Msuva amekataa kupokea mshahara

huo wa Sh milioni 9 akisema ni kidogo na alivyokuwa akitarajia. Difaa El Jajida ni timu ya Ligi Kuu nchini Morocco na msimu ujao itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kushika nafasi ya pili, mabingwa wakiwa Waydad Casablanca. Habari za uhakika kutoka Morocco zinaeleza, Msuva amesema mshahara huo ni mdogo.

“Tumeelezwa hivyo kwamba amekataa dola 4,000 ni kidogo. Pia timu yake haitaki kupokea dola 80,000 (takriban Sh milioni 177) kumuuza,” alisema Mohamed El Hamsi, mmoja wa mawakala nchini Morocco. “Mimi ushauri wangu waambie kuwa Tanzania haina soko huku Afrika ya Kaskazini, vizuri aje acheze na baada ya hapo

anaweza kutanua soko. “Naona si sahihi kukataa ofa hiyo, Yanga wamesema hadi dola 130,000 (zaidi ya Sh milioni 287). Nafikiri si sawa, ikiendelea hivyo baada ya siku chache tutaangalia Msenegal au Mmali mmoja ambao pia wanasubiri.” Juhudi za kumpata Msuva hazikufanikiwa kwa kuwa

yuko nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Cosafa. Hivi karibuni, Msuva alizungumza na gazeti hili na kueleza alikuwa na ofa tatu kutoka Afrika Kusini, Misri na Morocco na alikuwa tayari kwenda kokote kulingana na ofa.

 

Leave A Reply