The House of Favourite Newspapers

Msuva ashangazwa na matusi ya Azam

0

Msuva..[1]

Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Simon Msuva, amesikitishwa na kitendo cha wachezaji wa Azam cha kumtolea maneno machafu ya kumdhalilisha katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliozikutanisha timu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi Jumamosi.

Msuva alidai kuwa, wachezaji wa Azam walimtolea maneno machafu katika mchezo huo, mara baada ya kufanyiwa faulo na kipa wa timu hio, Aisha Manula na kusababisha penalti iliyopigwa na kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko lakini kipa huyo akaipangua.

Kitendo hicho kiliwaudhi wachezaji hao wa Azam na kuanza kumtolea maneno machafu wakimshutumu kuwa alijiangusha bila kuchezewa faulo na kipa huyo.

Maneno hayo ambayo Msuva hakuwa tayari kuyataja, alidai kuwa yamemsononesha.

“Ile ilikuwa penalti ya wazi kabisa kwa sababu Aishi alinifanyia faulo ya wazi ambayo kila mtu aliona, sasa nashangaa kwa nini wanitolee maneno machafu.

“Hata hivyo, sina cha kuwafanya ila wajiulize kama wangekuwa wao wangefanyaje,” alisema Msuva ambaye katika mchezo huo, aliingia kuchukua nafasi ya Malimi Busungu aliyeumia baada ya kufanyiwa faulo zaidi ya 10 na wachezaji wa Azam.

Leave A Reply