The House of Favourite Newspapers

MSUVA: LUGHA NI TATIZO KWANGU MOROCCO

0
Simon Msuva akikabidhiwa jezi.

KADIRI siku zinavyokwen­da, matajiri wa timu ya Difaa El Jadidi ya Morocco waliopata nafasi ya kumnasa nyota wa Yanga, Simon Msuva, wameendelea kuvutiwa na kiwango chake.

Kutokana na kuwa hatari kwenye kufunga mabao, kocha wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, Abder­rahim Taleb, amelazimi­ka kumbadilishia namba, amemtoa winga na kum­chezesha kama namba kumi.

Msuva ambaye ame­jiunga na klabu hiyo mwezi uliopita kwa mkataba wa miaka mi­tatu akitokea Yanga, ameendelea kuwa ki­vutio kikubwa kwa mashabiki wa Difaa kuto­kana na uwezo wake na kasi aliyonayo.

Msuva alianza kuwa­kosha mashabiki wa timu hiyo mapema, kwani katika mechi yake ya kwanza, siku moja tu baada ya kutua, alifunga, na sasa ana mabao saba katika mechi 10.

Kabla ya kuondoka Yanga, Msuva alikuwa ni mchezaji muhimu kikosini hapo ambapo msimu u l i ­opita aliibuka kinara wa ufungaji kwenye Ligi Kuu Bara akifunga mabao 14 sam­bamba na straika wa Ruvu Shooting, Abdul­rahman Mussa.

Championi Jumatatu limemtafuta Msuva na kufunguka mambo kad­haa ya maisha yake nda­ni na nje ya klabu hiyo.

C HAMPIONI : Unaweza kutueleza mapokezi yako baada ya kutua Morocco yaliku­waje?

MSUVA: Kiukweli mapokezi yangu hadi sasa ni mazuri kiasi kwamba inafikia wakati najihisi kama niko ny­umbani kabisa maana wachezaji na viongozi wangu wananipenda sana.

 

Msuva akiwa uwanjani.

CHAMPIONI: Kwa sasa unaishi kambini au umepangishiwa nyum­ba?

MSUVA: Hapa kwa sasa naishi katika ny­umba yangu mwenyewe ambayo nilikabidhiwa na klabu yangu baada tu ya ku­fi ka hapa Morocco.

CHAMPIONI: Unahisi mashabiki wa Difaa El Jadidi na makocha wako kwa jumla wanakuchuku­liaje tangu uanze maju­kumu yako?

MSUVA: Kiukweli naona wananizungumzia kwa mambo mazuri tu na hicho ndicho kitu pekee ambacho namshukuru sana Mungu kwani ha­masa na mwamko wanaonionyeshea ni mkubwa sana kwangu, hivyo in­afikia hatua naona kama nilichelewa kuja huku.

CHAMPIONI: Tan­gu umeanza kutekeleza majukumu yako unaona kuna tofauti ipi na Tan­zania?

MSUVA: Tofauti zipo maana huku ni nje ya nchi yangu niliyokuwa nimeizoea, nimeku­tana na vitu tofauti sana huku hasa ninapokuwa uwanja­ni na hata nikiwa nje ya uwanja kuna vitu vizuri ambavyo siku­wahi kuvipata, hivyo nazidi kujifunza kila kukicha.

CHAM­PIONI: Changamo­to zipi una­zokutana nazo na kwa namna moja zinakuwa kero kwako?

MSUVA : Changamo­to zipo, si unajua huku nipo ugen­ini! Kuna vitu nilikuwa nimezoea sana nikiwa Bongo, kama lugha yangu ya Kiswahili ambayo ndiyo nilikuwa naitu­mia kwa asil­imia kubwa na mara chache Kingereza nakijuajua ki­dogo, lakini changamoto kubwa huku wengi wao ha­wajui kabisa Kingereza, sana­sana wanazun­gumza Kiarabu na Kifaransa tu, hivyo kuna muda inaniwia vingumu sana kwenye ma­wasiliano hasa kwa lugha hizi mbili am­bazo sizijui.

CHAMPIONI: Ukiwa haupo na timu unafanya nini?

MSUVA: Huwa narudi kupumzika kwangu. Nitaenda wapi na sina ninapopajua?

CHAMPIONI : Chakula cha huko kikoje, na wewe un­akula nini?

 

Msuva baada ya kusaini.

MSUVA: Ni ngu­mu kutaja chakula chao (maana hakiju­likani ukikiona). Mimi nakula zaidi wali lakini huku unapikwa to­fauti na tulivyozoea. Huwa nakula pia po­tatoes (viazi), kuku au samaki. Na asubuhi ni mikate, maziwa na mayai.

CHAMPIONI: Je, hapo kwenye klabu yako kuna mchezaji mwingine yeyote wa huku Afrika Masha­riki?

MSUVA: Hakuna mchezaji yeyote kuto­ka Afrika Mashariki, ila wapo watatu wa­natoka Afrika, kama kuna mmoja anatokea Cameroon, wengine Senegal na Gabon.

CHAMPIONI : Ligi ya huko inaanza rasmi lini, na ume­shaanza kubaini uto­fauti?

MSUVA: Ligi inaanza Septemba mwishoni, pia to­fauti ya ligi ya huku na Bongo ipo kidogo tu na siyo sana, zaidi ni uendeshwaji wake ndiyo una tofauti kubwa kwani huku hakuna mambo ya ubabaishaji kama ilivyo kwetu ambapo ratiba imekuwa haii­shi kupanguliwa-pan­guliwa.

CHAMPIONI : Wapinzani wakubwa huko ni timu gani kama ukilinganisha na huku zilivyo Simba na Yanga?

MSUVA: Timu yetu ya Difaa El Jadidi na Wydad Casablanca zina upinzani mkubwa kama ilivyo Simba na Yanga, lakini pia zinapokutana Raja Casablanca na Wydad Casablanca, hii ndiyo derby pekee ambayo mashabiki huwa ha­walali usingizi wakisi­kia timu hizi zinaku­tana.

CHAMPIONI : Huko unacheza nafasi gani?

MSUVA: Tangu kocha wangu amen­iona siku ya kwanza aliniambia nicheze namba 10, maana huyu kocha kasema mimi najua sana kufunga, kwa hiyo hawezi kunicheze­sha pembeni, badala yake kaniweka pale kati ili niwe huru ku­fanya lolote na waka­ti wowote ule hasa nikitaka kufumania nyavu.

MAKALA: MUSA MATEJA TANZANIA

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply