Mtabiri: Chama kitakachoshindwa ndiyo utakuwa mwisho wake

edoloNa Mwandishi Wetu
MTABIRI maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein amesema chama cha siasa kati ya vyama viwili vikubwa nchini kitakachoshindwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wake.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum jana, Maalim Hassan alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) vina wakati mgumu na vinashikwa kinyota kutokana na wagombea wake kutofautiana.

01“Mwaka huu ulianza Alhamisi ambayo kinyota asili yake ni moto na wagombea wao, Edward Lowassa wa Chadema jina lake linaanzia L , nyota yake ni Mshale ambayo asili yake ni moto na (Dk. John) Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi ambaye jina lake linaanza na M, nyota yake ni ya samaki ambayo asili yake ni maji, majina hayo yana maana sana kinyota.

“Kwa kawaida maji huzima moto lakini pia maji yakizidi, moto huzimika, hii maana yake ni kwamba chama ambacho mgombea wake ana nyota asili ya maji kikishinda, basi kile cha mgombea ambaye asili yake ni maji kitakufa na moto ukizidi unaweza kukausha maji, hivyo kiutabiri chama kitakachoshindwa kitakufa moja kwa moja au kufifia sana,” alitahadharisha.

Chadema mwenyekiti wake ni Freeman Mbowe wakati CCM mwenyekiti wake ni Rais Jakaya Kikwete.

Uchaguzi mkuu nchini unatarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kwamba matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72.

Loading...

Toa comment