The House of Favourite Newspapers

MTALII AFIA Chini ya Bahari ZANZIBAR Akimchumbia Mpenzi Wake! (Picha +Video)

Kenesha Antoine akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Steven Weber jr.

MTALII mmoja aliyejulikana kwa jina la Steven Weber Jr, alifariki Dunia hivi karibuni akiwa chini ya Bahari alikoenda kumvisha pete mchumba wake, Kenesha Antoine wakati wa likizo.

Kulingana na mtandao wa Sky News, Steven Weber na Kenesha Antoine walikuwa wakiishi katika hoteli moja ya mbao ambayo ipo chini ya maji ya Bahari huko Visiwani  Zanzibar,  ili kuwawezesha kuona kilichopo maji.

Picha zimeonyesha wakati bwana Weber kutoka eneo la Baton Rounge mjini Luoisiana Marekani, alivyoogelea hadi katika dirisha moja lililopo chini ya maji kabla ya kushika karatasi akimuomba  Antoine akubali kufunga naye ndoa.

Karatasi hiyo ilisoma kwa tafsiri isiyo rasmi: “Siwezi kuzuia pumzi zangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokupendea lakini kila kitu ninachokupendea nakupendea kila siku”.

Bwana Weber baadaye aliibadilisha karatasi hiyo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande mwengine yaliosema: “Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu? Utafunga ndoa nami???.

Kulingana na mtandao wa Sky News, baadaye alitoa pete ya uchumba kutoka katika mfuko wake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo.

Bi Antoine naye alichapisha picha za kisa hicho katika facebook ambapo anaonekana akifurahia pamoja na tamko lake: Ndio! Ndio! Ndio!.

Lakini mrembo huyo baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake amefariki.

Bi Antoine alisema kwamba hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini.

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilisema kwamba mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchini Tanzania lakini hakuna maelezo zaidi yalioripotiwa.

Bi Antoine aliandika: “Hakuna maneno yatakayotoa heshima kwa mpenzi wangu Steven Weber Jr.

“Hukutokezea tena kutoka kina hicho cha bahari hivyo basi hukuweza kusikia nikikubali mara milioni kwamba ndio nitafunga ndoa nawe”!

”Hatukuweza kukumbatiana na kusherehekea mwanzo wa maisha yetu yaliosalia, baada ya siku bora zaidi katika maisha yetu kuwa mbaya zaidi”.

”Nitajaribu kujifariji kwa kuwa tulifurahia siku zetu za hivi karibuni na kwamba sote tulikuwa tumejawa na furaha wakati wetu wa mwisho”.

Comments are closed.