The House of Favourite Newspapers

MTALII AUAWA KWA KUKANYAGWA NA TEMBO

Tembo

Mtalii wa Ujerumani amefariki baada kukanyagwa na tembo alipokuwa akijaribu kumpiga picha nchini Zimbabwe.

Mamlaka nchini humo imethibitisha kuwa mkasa huo ulifanyika katika mbuga ya kitaifa ya Mana Pools na kwamba mwanamke huyo alifariki siku hiyo kutokana na majeraha aliyopata. Mwanamke ambaye jina lake halijabainika alikua miongoni mwa kundi la watalii waliyokutana na tembo walipoingia katika mbuga ya wanyama. Visa vya watu kushambuliwa na tembo vimekithiri sana nchini Zimbabwe.

 

Mara nyingi wanyama hao huvamia mashamba wakulima.Msemaji wa Mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori nchini Zimbabwe,Tinashe Farawo, amesema mamlaka hiyo haijabainisha chanzo cha shambulio hilo. “Tunawaomba watu kukaa mbali na wanamapori na kuwa waangalifu wanapokutana nao”.Tembo

Katika tukio jingine sawia na hilo mwaka jana, raia wa Zimbabwe aliuawa na tembo alipokua akijaribu kuwaelekeza sehemu ya wazi ili awezi kuwapiga picha Zimbabwe ni taifa la pili duniani lililo na idadi kubwa ya tembo. Kwa mujibu wa sensa ya tembo ya mwaka 2016 taifa hilo lina tembo elfu 82,304

Comments are closed.