The House of Favourite Newspapers

Mtambule: Sera Nzuri, Miundombinu na Usimamizi Vimevutia Wawekezaji Nchini

0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambuke, amesema kuwa matokeo mazuri ya sera, na miundombinu, usimamizi ni chanzo cha kuvujitia wa wawekezaji hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule wakati wa Uzinduzi wa Mgahawa wa KFC katika Eneo la Magomeni Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Februari 15, 2024. Amesema kuwa Serikali ya wilaya ya Kinondoni itatoa ushirikiano mzuri katika ulinzi, Usalama na usafi ili waweze kutoa huduma bila kikwazo chochote.

Amesema kuwa vijana sio 40 wamepata ajira kufuatia kufunguliwa kwa mgahawa wa 10 hapa nchini hilo ni fahali kwa Tanzania kutokana na namna serikali ya Tanzania inavyofanya mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

“Tunaona huduma zuri ya chakula inaenda kupatikana sasa Magomeni, watu wengi wanakuja kujifunza namna ya kutengeneza chipsi kutoka maeneo mbalimbali na kujifunza namna ya utoaji wa huduma inavyotolewa kwenye migahawa ya KFC hii ni fahari kwa watanzania kupata ujuzi mbalimbali.” Amesema

Dough Works Limited imetangaza ushirikiano wake na Kampuni ya Usambazaji wa Mafuta na Vilainishi ya vyombo vya moto ijulikanayo kama Total Energies wakati wa uzinduzi wa mgahawa wao wa 10 wa KFC uliofunguliwa katika Kituo cha Huduma ya Mafuta cha Total kilichopo Magomeni, Mapipa kwa lengo la kupanua wigo wa uwepo wa migahawa inayotoa huduma ya haraka ya Chakula nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works Limited, Vikram Desai amesema kuwa uzinduzi huo imekuwa ni miezi ya furaha na mafanikio kwa KFC na Dough Works kwa ujumla.

“Tukiwa tumeadhimisha Miaka 10 ya KFC nchini Tanzania na sasa kufungua KFC yetu ya 10 nchini kwa ushirikiano na Kampuni ya TotalEnergies ni hatua muhimu kwetu. KFC ni chapa ya kimataifa, na yenye maduka 23,000 katika zaidi ya nchi 140 duniani kote. Tunafurahi kuisambaza migahawa yetu ya KFC ulimwenguni kote na katika jamii zetu na kuendelea kutimiza ahadi yetu ya kutoa chakula chenye ubora na cha uhakika nchini Tanzania. Zaidi ya hayo, tunafurahi kuungana na mshirika mwingine ambaye atakuwa msaada mkubwa katika ukuaji wetu ambaye si mwingine bali ni TotalEnergies, na tunatarajia kufanya miradi mingine zaidi pamoja katika siku zijazo.” Amesema.

Kwa Upande wa Makamu wa Rais wa TotalEnergies kwa Afrika Mashariki na Kati, Olagoke Aluko, amesema kuwa Vituo vya TotalEnergies vitatambulika kwa kutoa huduma ya pamoja ambayo kwa sasa unaweza kushuhudia hilo katika kituo cha Magomeni ambapo mteja anaweza kupata huduma zote muhimu kutoka kwa huduma ya upatikanaji mafuta hadi huduma za gari, huduma za ATM na sasa huduma ya chakula cha haraka tena kile kinachopendwa na maarufu kwa sasa duniani kote na kufunguliwa kwa mgahawa huu ni ishara ya uwepo wa mgahawa wa KFC wa 10 nchini Tanzania.

Habari @imeldamtema

Leave A Reply