Mtamuona Mume Wa Dayna Akishamuoa

Mwanaisha Nyange ‘Dayna’.

MWANAMUZIKi anayefanya poa kunako uwanda wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna’, amefunguka sababu ya kuficha uhusiano wake na kwamba mumewe ataonekana akishamuoa.

 

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Dayna amesema hapendi kuweka uhusiano wake hadharani kutokana na malezi aliyolelewa hivyo hadi wakati ufike wa kuchumbiwa na kuolewa.

“Sipendi sana kuweka uhusiano wangu hadharani, naweza kusema ni kutokana na malezi niliyolelewa. Kwamba nianze kutangaza, nawaza familia yangu itaniangaliaje ila wakati utakapofika wa familia kujuana, nikachumbiwa, ndiyo nitaweka wazi.

 

Na mwanaume wangu atakayenioa nitamposti sana japo natamani kutoka katika maisha ya usiri,’’ amesema Dayna ambaye kwa sasa anatamba na mkwaju wake mpya wa Homa.

STORI: HAPPY MASUNGA

Toa comment