The House of Favourite Newspapers

Mtandao wa Kijamii Wampeleka Mbunge Jela

 

MBUNGE na aliyekuwa waziri wa zamani wa michezo wa Ivory Coast, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kusambaza taarifa za uongo kupitia ukarasa wake wa Twitter.

 

Alain Lobognan aliandika katika ukurasa wake wa Twitter tarehe 9 Januari mwaka huu kuwa mkuu wa upelelezi ametoa tamko la kukamatwa kwa mbunge mwenzake, taarifa ambayo ilizua gumzo na fujo  miongoni wa wafuasi wa mbunge huyo.

 

Lakini mkuu wa upelelezi alikanusha kutoa tamko hilo kama alivyoandika Lobognan katika ukurasa wake wa Twitter.

 

 

Mbunge huyo ambaye yupo katika mgomo wa kula siku ya kumi sasa anasema kuwa kesi yake imeingiliwa kisiasa.  Mwanasheria wake, Bi Affoussiata Bamba Lamine, amesema wana mpango wa kukata rufaa.

 

Ameongeza pia kuwa kesi ya mteja wake imeingiliwa kisiasa, na kusema kuwa analengwa kwa sababu ya ukaribu wake na waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa pia kiongozi wa zamani wa waasi, Guillaume Soro.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.