The House of Favourite Newspapers

Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Indonesia

 

RAIA wa Tanzania aliyetambulika kwa jina la Abdul Rahman Asman anadaiwa kukamatwa huko Bali nchini Indonesia akiwa na madawa ya kulevya aliyokuwa ameyameza tumboni.

 

Maofisa katika Uwanja wa Ndege wa Bali wameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa Mtanzania huyo alikamatwa Januari 30, mwaka huu (2019).

 

Wamesema alipopekuliwa alibainika alikuwa amemeza madawa hayoa mbayo, hata hivyo,  hayakufafanuliwa ni ya aina gani, lakini baadhi ya ripoti zilisema madawa aliyokutwa nayo yanafahamika kwa jina la methamphetamine.

 

Mtandao mmoja umeripoti kuwa:  “Mtanzania huyo alikamatwa Bali akiwa na kilo kadhaa za dawa hizo.”

 

Taarifa zaidi zimedai kuwa alipofanyiwa uchunguzi wa X-ray na CT scan aligundulika kuwa na paketi kadhaa za plastiki na ndani yake kukiwa na unga.

 

 

Haikulezwa ni lini atapandishwa mahakamani na haikufahamika mara moja iwapo upande wa mashtaka utataka mtuhumiwa huyo ahukumiwe adhabu ya kifo. Indonesia inatajwa kuwa ni moja ya mataifa duniani yenye sheria kali dhidi ya makosa yanayohusiana na usafirishaji wa madawa ya kulevya.

 

Kuna mlolongo wa watuhumiwa wanaosubiri adhabu ya kifo wakiwamo raia wa Uingereza, Marekani na wengine kutoka Afrika Magharibi ambao wamenyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.