Mtanzania Ashinda Tuzo Ya Kuhamasisha Vijana Moscow
Mtanzania Mohamed Mansour ameshinda tuzo ya kuhamasisha vijana wa Afrika nchini Urusi katika masuala ya Taaluma (Elimu) na Maendeleo ya Jamii (Community Development) kutoka Shirika la vijana wa Kiafrika lisilo la Kiserikali (NGO) la Youth of Large Exploit (YOLE), katika hafla yao iliofanyika mjini Moscow usiku wa kuamkia leo.
Alichokisema mtanzania huyo baada ya kushinda tuzo hiyo: “Kwa uwezo wa Mungu, pamoja na tunzo hii ya leo tayari inakua ni mara ya pili kutambuliwa Kimataifa kwa mwaka huu wa 2019, mwezi Januari nilichapishwa na kutambuliwa Kimataifa kama Mtanzania maarufu zaidi katika Watanzania waliowahi kusoma vyuo vya Sovieti ya Urusi na katika jarida la Kimataifa (Encyclopedia) la Wahitimu wote wa kigeni waliosoma nchini Urusi yani SOYUZ Alumni.
“Nawashukuru sana viongozi wa shirika la YOLE na pia Chama chetu Cha SOYUZ Alumni Association of Tanzania walioniamini ili kuwawakilisha Kimataifa kama Balozi wao.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania!
Ahsante sana!,”alisema Mansour.
Comments are closed.