Mtanzania Atikisa Hollywood, Asimulia Safari Yake Katika Utengenezaji Filamu Ya Mufasa The Lion King – Video

Mtayarishaji na mzalishaji wa video na filamu mwenye uzoefu wa muda mrefu nchini Tanzania, Mussa Ally, maarufu kama Kaka Mussa, ni Mtanzania pekee aliyepata bahati ya kushiriki katika uaandaaji wa filamu ya Hollywood Marekani ya MUFASA: The Lion King, ambayo kwa sasa imeliteka soko la filamu duniani amefunguka kupitia Global TV na kusema kuwa, dili la utayarishaji wa kazi ya MUFASA: THE LION KING lilianzia mwaka 2019.