MTANZANIA THOMAS MLUGU ATINGA 16 BORA LEO
Thomas Andrew Mlugu amezidi kushika vichwa vya habari huko jijini Paris hii leo baada ya kuibuka kidedea kwenye mchezo wa Judo ambapo ameweza kufanya vizuri hatua ya makundi kwenye michuano ya Olympics 2024.
Siku ya leo tarehe 29 Julai 2024, Mtanzania Thomas Andrew Mlugu ameanza vyema mchezo wake wa kwanza kwenye mashindano ya Olimpiki ambayo inaendelea huko Ufaransa ikiwa ni mashindano ya 33 ya majira ya joto za Paris 2024 toka yaanzishwe.
Thomas Mlugu ambaye ana uzito wa 73kg amemtoa Ippon (KO ya Judo) mpinzani wake William Tai Tin ambaye ni raia wa Samoa ambaye alishikwa vilivyo na Mlugu toka mwanzo wa pambano. Jisajili na usuke jamvi la ushindi.
Inasemekana kwamba Thomas ndiye Mwafrika pekee ambaye ameshinda katika awamu hii kati ya Waafrika waane ambao walicheza pambano leo hii katika ukumbi wa Champs-De-Mars huku wote hao wakiwa wamepangwa kwenye Kundi C.
Michezo ya Olympic 2024 inaendelea leo hii ambapo Taifa la Tanzania litamtazama Thomas Andrew Mlugu anayepeperusha vyema bendera ya Tanzania. Cheza pia michezo ya Kasino mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roulette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.
Baada ya kushinda sasa Mlugu aliweza kuongea na kusema kuwa licha ya kumaliza pambano hilo, ameumia goti lake la kushoto akiwa kwenye pambano lakini hiyo haitaweza kumfanya akate tamaa na kuwaangusha Watanzania ambao wanamtegemea kuipeperusha vyema nchi yake.
Thomas Mlugu baada ya kupata ushindi huo wa hatua ya makundi, sasa Mlugu ametinga kwenye hatua ya 16 bora, kama akishinda atakipiga Robo Fainali, kisha Nusu Fainali, na Fainali ambazo hizi zote zinatarajiwa kupigwa siku ya leo hapo baadae.
Mtanzania huyo mechi yake inayofuata atapambana na Mfaransa Joan-Benjamin Gaba ambapo jioni ya leo washindi katika uzito anaocheza Mlugu watavalishwa medali za ushindi. Beti na Meridianbet sasa.
Usikose uhondo huu wa bwana Mlugu akiwania ubingwa wa Judo na michezo mingine kibao ya Olimpics inayoendelea huko jijini Paris. Meridianbet inakupa fursa ya kuwa bingwa kwa kubashiri michezo hii ya Olympics 2024.