The House of Favourite Newspapers

MTAZAMO WA WADAU KUHUSIANA NA Infinix HOT 6

Baada ya ujio wa Infinix HOT 6 na kufanya vizuri sokoni kutokana muonekano na uwezo wake lakini pia wadau wameweza kuongelea upande wake wa pili na kuweza kuyawasilisha kama ifuatavyo.

Infinix HOT 6 ni simu iliyoboreshwa zaidi katika vionjo vya muziki kama vile spika mbili ikiwa na maana imemlenga zaidi mpenzi wa muziki hivyo basi tulitegemea Infinix HOT 6 kuja ikiwa na headphone kama ilivyo kwa TECNO BOOM J8 na si vi earphone.

 

 

Na kulingana na teknolojia kuendelea kukua tulitegemea Infinix HOT 6 yenye kasi ya 4G lakini hapa tumeona kampuni ya simu ya Infinix wameturudisha kwenye mfumo wa 3G tunategemea mabadiliko ya mtandao katika matoleo yanayokuja.

 

Sifa nyengine ambayo ni kujivunia ni uwezo wa kamera wa simu, inakamera nzuri  ya megapixel 13 nyuma ikiwa na flashi mbili na megapixel 5 mbele ikiwa na flashi. Infinix HOT 6 inakupa uhakika wa picha nzuri wakati wowote ule hata katika mwanga hafifu. Lakini pia muonekano wake unavutia sana ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 kwa nchi 6.0.

Katika upande wa Android ipo vizuri sana Infinix HOT 6 imekuja na Android 8.1 yenye kuzuia uishaji wa chaji katika simu kwa haraka lakini pia imesaidia simu kuwa na ‘application’ mpya kama vile face id lakini pia imeongeza ufanisi katika simu.

 

Kuhusiana na uwezo wa processor sio kama vile tulivyotegemea tumeona simu nyingi zikija na Qualcomm spandragon kama ilivyo kwa toleo la  awali la Infinix HOT S3 lakini kampuni imeturudisha nyuma na MTK6580 processor ya 1.3 ghz quard core.

Na uhakika wa kudumu na chaji ni mkubwa inabetri ya ujazo wa 4000mAh inaweza kuhimili matumizi ndani ya siku mbili pasipo kuzima.

Comments are closed.