The House of Favourite Newspapers

MTCC Kuja na Mkakati Mpya Kuboresha Maendeleo ya Bandari

0
Marekebisho na ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam yanaendelea

KITUO cha Ushirikiano wa Teknolojia ya Bahari, Maritime Technology Cooperation Centre (MTCC) ambacho kina wanachama kumi, Tanzania ikiwepo, wamekuja na mkakati kazi kwa ajili ya kuongeza maendeleo katika sehemu ya magharibi ya Bahari ya Hindi bila kuathiri shughuli zingine za kijamii na kiuchumi.

 

Mpango huo unakuja wakati takriban nchi zote kumi wanachama wa MTCC zipo katika mkakati wa kuimarisha uwekezaji ili kuvuna mapato zaidi kutokana na uchumi wa bluu, ambayo pia inajumuisha ujenzi wa bandari.

Haya yanajiri wakati ufukwe wa Tanzania wenye urefu wa kilomita 1,420 katika ukanda wa pwani ya Hindi ukijishughulisha na uboreshaji wa miundombinu ya usafiri, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa bandari na miundombinu mingine kama barabara, reli na majengo.

 

“Tumekuja na mkakati huu kama waraka wa kuziongoza nchi wanachama wa MTCC kukabiliana na athari za muda mrefu za shughuli za maendeleo ya bandari kwa wenyeji, hii ina maana kwamba mara bandari mpya inapoendelezwa, jumuiya za wenyeji zinaweza kuathiriwa kijamii, kiuchumi na kitamaduni,” alisema Dk Arthur Tuda, Katibu Mtendaji wa Chama cha Sayansi ya Bahari ya Hindi Magharibi (WIOMSA).

 

Mkakati kazi kwa ajili ya kuongeza maendeleo katika sehemu ya magharibi ya Bahari ya Hindi

Akifafanua, Dk Tuda alisema jamii za wenyeji zinaweza kuathiriwa kiuchumi kwa kukata misitu na kuchukua ardhi ili kuendeleza bandari, hivyo kudumaza shughuli zao za kiuchumi.

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

 

Leave A Reply