The House of Favourite Newspapers

Mtemvu alivyotoa siri za Nyerere- 11

0

HISTORIA ya Zuberi Mtemvu na Mwalimu Julius Nyerere inaendelea:

Vita kati ya Mtemvu na Nyerere inasemekana ilikuwa imeanza siku nyingi kama tulivyoona huko nyuma.

Mtu pekee aliyekuwa akipoza ugomvi huo ni kada wa Tanu wa enzi hizo, John Rupia ambaye alikataa kutimuliwa Mtemvu ndani ya chama, kwa hiyo Nyerere hakufanikiwa lengo lake.

Mwalimu Nyerere alitibuliwa na Mtemvu miaka michache kabla ya uhuru. Mtemvu, akiwahutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Karl Marx mjini Leipzig, Ujerumani ya Mashariki, alibashiri kuwa kutolewa kwa uhuru wa Tanganyika kwa uongozi wa Tanu, hakutabadili chochote kwa kuwa wanaoingia madarakani wameamua kushirikiana na walewale wanyonyaji wa zamani.

Alisema hiyo itavunja nguvu za wazalendo na matumaini yao ya kutafuta uhuru. Nyerere aliposikia hayo alimchukia Mtemvu na akawa hataki kuzungumza naye.

Siku za mwisho za mzee Mtemvu alikuwa anatoka Morogoro kuja nyumbani kwa mwanaye Abbas Mtemvu, aliyekuwa bosi wangu katika Gazeti la Baraza na nilikuwa nakutana naye na kumdodosa haya ninayoyaandika leo.

Nyakati za jioni mzee Mtemvu alikuwa akipenda kukaa nje ya nyumba yake kupunga upepo. Nikifika pale nilikuwa nakwenda kumwamkia na hapo tunaanza gumzo.

Alikuwa akinishinda kwa hoja basi mimi humchokoza kwa kumwambia, “Lakini baba unajua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika imekuweka wewe katika kundi la wasaliti?”

Itaendelea wiki ijayo.

Leave A Reply