Mtemvu alivyotoa siri za Nyerere- 12

Naendelea na makala hii inayozungumzia jinsi Mtemvu alivyotoa siri za Nyerere miaka ya nyuma akiwa katika utawala wake. Sasa endelea…

Mzee Zuberi Mtemvu nilipoonana naye nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam alinisimulia mengi.

Alinieleza historia ya Tanu na kwamba yeye alikuwa mmoja wa wazalendo waliotayarisha mkutano wa Tanu wa kwanza uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo, Mnazi Mmoja Dar ambao haukuhudhuriwa na watu zaidi ya ishirini.

Alisema mkutano wa uzinduzi wa Tanu ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 na akanitajia muongoni mwao walikuwepo Mwalimu Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio na Denis Phombeah.

Alisema tangazo la mkutano huo lilichapishwa katika gazeti la Ramadhani Mashado lililokuwa likiitwa Plantan Zuhra.

“Wote tulikuwa wahamasishaji wakubwa wa umma lakini miaka minne baadaye tulitupana mkono na Mwalimu Nyerere na nikaanzisha chama cha upinzani,” alisema mzee Mtemvu.

Mtemvu alisema alipohama Tanu kuunda chama chake cha upinzani, Said Chamwenyewe alitoka Tanu na kujiunga naye. “Umuhimu wa Chamwenyewe ni kuwa Msajili wa Vyama alipokataa kuisajili Tanu kwa kisingizio kuwa haina wanachama, marehemu Abdulwahid Sykes alimpa Chamwenyewe kitabu cha rejesta na kadi za Tanu akamuomba aende Rufiji, Pwani akatafute wanachama,” alisema.

Itaendelea wiki ijayo.

Loading...

Toa comment