The House of Favourite Newspapers

MTENDAJI MKUU MAHAKAMA AKAGUA MIRADI YA UJENZI MAHAKAMA NCHINI

Picha ya pamoja ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama , viongozi wa Mahakama Mkoa wa Kigoma na wakandarasi wa Masasi Construction wakiwa mbele ya jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma linaloendelea kujengwa.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw Hussein Kattanga (wa kwanza kulia) akikagua kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Mahakama ya Wilaya Buhigwe ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma kwa wananchi mkoani Kigoma.

Mtendaji Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma Bw. Moses Mashaka akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi mbele ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Bw. Leonard Magacha.

Hali ya jengo la Mahakama kuu kanda ya Kigoma lilipofikia

 

 

Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Husssein Kattanga amefanya ziara mkoani Kigoma na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu lililoanza kujengwa rasmi Oktoba 28, 2017 chini ya mkandarasi Masasi Construction Co Ltd.

 

 

Ujenzi huo wa Jengo la Mahakama Kuu utasogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi wa Mkoa huo kwani wamekuwa wakisafiri kutoka Kigoma kwenda Tabora kufuata huduma za Mahakama Kuu.

 

 

Katika ziara hiyo Mtendaji Mkuu wa Mahakama alipata fursa ya kutembelea mahakama ya Wilaya Kasulu na kukagua ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Kasulu inayotegemewa kumalizika mwezi April 2019 chini ya Mkandarasi M/S Molad Tanzania LTD.

 

 

Ujenzi wa Mahakama mbalimbali nchini unalenga katika kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi na vilevile ni utekelezaji dhahiri wa nguzo ya pili ya mpango mkakati wa Mahakama (2015/2016-2019/2020) ya upatikanaji wa haki kwa wakati.

 

 

Aidha ujenzi wa jengo hilo la Mahakama na unaotarajiwa kukamilika mwezi Juni 2019 utawezesha uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka mbalimbali na kuimarisha matumizi ya vifaa vya TEHAMA katika huduma ya utoaji haki.

 

 

Picha na Festo Sanga, Kigoma

Comments are closed.