The House of Favourite Newspapers

Mtetezi Maarufu wa Mashoga Afariki Dunia

 

MWANAHARAKATI wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya, Binyavanga Wainaina, amefariki. Nduguye James Wainaina amethibitisha kwa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC).

 

Wainaina amefariki akiwa na umri wa miaka 48 na nduguye  amesema kuwa familia yake inataka kusherehekea maisha yake baada ya mwandishi huyo wa Kenya kufariki usiku wa Jumanne alipokuwa akiugua

”Tunasherehekea maisha yake, tunaangazia suala hili kibinadamu.  Turuhusu ubinadamu kung’aa, kwa kuwa watu wanaomboleza”alisema James akizungumza na mwadishi wa BBC, Peter Mwangagi.

 

”Alifariki jana usiku katika hospitali moja alipokuwa akiugua. Lakini hicho ndicho kilichopo kwa sasa, tunajaribu kukubaliana na habari hiyo”, aliongezea.

 

James amesema  ijapokuwa habari za kifo cha nduguye tayari zimejaa katika mitandao ya kijamii, familia inajaribu kuwaelezea wale wasiojua.

James alisema kuwa Binyavanga hajawahi kuwa katika afya nzuri katika kipindi cha miaka michache iliyopita na hali yake ilikuwa imedorora katika kipindi cha kati ya miezi miwili au mitatu.

Hata hivyo,  alikataa kufichua ugonjwa uliosababisha kifo cha nduguye.

 

Wainaina, alikuwa miongoni mwa Wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

 

Tangazo hilo lilimfanya Binyavanga kuwa mmoja wa Waafrika mashuhuri kujitokeza hadharani ambapo  alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliowiana na siku ya kuzaliwa kwake.

 

Comments are closed.