Mti wa Maajabu, Ukiupanda Mtu Anakufa, Mke Hazai – Shehe Aanika – Video

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni! Mti unaoitwa ‘Germany Tree’ unaofahamika zaidi kwa jina la Mti Chonganishi, ni aina ya mti ambao hupendwa sana na watu na hupandwa kwenye majumba ya watu.

 

Mti huo unasemekana kuwa na tabia za ajabu yaani ukiupanda nyumbani kwako basi nyumba hiyo haitakauka vibweka ikiwa ni pamoja na watu kufariki, magonjwa, migogoro isiyoisha.  Kama umepandwa maeneo ya shuleni, basi wanafunzi wanaweza kupata balaa la kuangukaanguka.

 

Global TV imepita mtaani na kushuhudia nyumba kadhaa zikiwa zimeupanda mti huo na kuzungumza na wahusika, ambapo majirani na watu mbalimbali wanafahamu vizuri historia ya mti huo.

 

Aidha, imezungumza na Sheikh Shariff Majini, ambaye ameelezea kwa kina zaidi juu ya mti huo na kutaja aina mbalimbali za miti ambayo ni hatari kuipanda majumbani.

 

Hii ni sehemu ya kwanza ya historia ya mti huu, sehemu ya pili itakujia kesho Agosti 13, 2019, saa 12 jioni.


Loading...

Toa comment