Kartra

Mtibwa, Kagera Hali Tete Ligi Kuu Bara

Klabu ndugu za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zimepoteza mechi zao za ligi kuu Tanzania bara jana na hivyo kuleta mashaka ya kubakia kwa msimu ujao.

Mtibwa ilipoteza 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mechi iliyochezwa mapema saa 8 :00 mchana katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, magoli ya wageni yalifungwa na Abdulaziz Makame naTariq Seif katika kipindi cha kwanza na lile la wenyeji lilifungwa na Kelvin Sabato katika kipindi cha pili.

 

Kagera Sugar wao walipoteza 2-1 dhidi ya Biashara Mara kwenye mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa sana uliyochagizwa na kocha Francis Baraza kuzifundisha timu zote mbili hizi kwa awamu tofauti kulifanya morali ya mechi kuwa juu sana.

 

Kupoteza kwa Mtibwa na Kagera kunaziweka timu hizi zenye nasaba katika wakati mgumu wa kushuka daraja, kwa sasa Mtibwa ipo katika nafasi ya 14 kati ya timu 18 na Kagera Sugar ipo katika nafasi ya 16 kati ya timu 18 na kwa mujibu wa kanuni timu ,4 zinashuka moja kwa moja msimu huu.


Toa comment