LICHA ya kupoteza kwa mabao 3-0 katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa ugenini, uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar umefunguka kwamba lengo lao walilolikusudia ni kugeuza matokeo hayo wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Mtibwa ilipoteza mechi yake mbele ya KCCA ya Uganda kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kwa mabao 3-0 wakiwa wanacheza ugenini nchini Uganda. Mtibwa watalazimika kushinda zaidi ya mabao 3-0 ili kusonga mbele.
Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru amesema kwamba tayari benchi la: “Tumekubali tumepoteza mechi yetu ya ugenini lakini hilo halitufanyi kwamba tukaona tayari tumeshatoka kwenye michuano hii. Bado tuna nafasi na tutaifanyia kazi.
“Makocha wamechukua makosa yote na tuseme kwamba kwenye mechi ya marudiano tutafanya kila tuwezalo ili tubadilishe matokeo hayo na tusonge mbele kwenye michuano hii mikubwa hapa Afrika.”
Katika hatua nyingine, straika wa Mtibwa, Juma Liuzio amesema: “Tuliwasoma wapinzani wetu licha ya kuwa wazuri lakini kipindi cha pili walichoka sana, hivyo tutatumia udhaifu wao huo ili tupate ushindi hapa nyumbani na tusonge mbele.”
Comments are closed.