Mtihani Darasa la 7, DED Aagiza Kuvunja Makundi Yote WhatsApp

Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma imevunja makundi yote ya ‘WhatsApp’ ya waratibu elimu msingi ili kuepuka udanganyifu katika mitihani ya darasa la saba inayofanyika kesho na keshokutwa.

Katika barua hiyo iliyoandikwa kwa waratibu kata elimu wote Agosti 19, 2019 na kusainiwa na Josephat Ambilikile kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo imewataka waratibu elimu kata wote kuvunja makundi hayo.

Makundi hayo ni yale yanayotumika kutoa au kupokea taarifa zozote zinahusiana na utendaji wa taaluma.

Ambilikile amesema pia ofisi imebaini kuwepo kwa makundi ya WhatsApp katika halmashauri hiyo yanayotoa taarifa mbalimbali za kielimu na kijamii.


Loading...

Toa comment