The House of Favourite Newspapers

Mtitu: pale leaders panaua film

0

MTITU42Staa wa Filamu za Kibongo, William Mtitu ‘Mtitu’.

Hamida hassan

Staa wa Filamu za Kibongo, William Mtitu ‘Mtitu’ ameonesha kuwashangaa mastaa wanaoshinda Viwanja vya Leaders wakinywa pombe na kupiga stori wakati tasnia ya filamu inaanguka.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Mtitu alisema kuwa huu si wakati wa kubweteka na kutumia pesa kwa anasa, anacho washauri wasanii ni kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa jahazi ambalo sasa linaelekea kubaya.

“Yaani pale Leaders panaua sanaa yetu ya uigizaji, kuna siku utaona wasanii wakubwa waliokuwa na majina makubwa mjini wameanguka kwa sababu sasa wanashindwa jinsi ya kuokoa janga hili ambalo ni kubwa na linahitaji watu kubadilika,” alisema Mtitu.

Leave A Reply