Mtoto Adaiwa Kutekwa Na Mtu Asiyejulikana ”Alimfuata Shuleni – Video
Mtoto Angel Kamugisha (6) mkazi wa Kinondoni Shamba, amechukuliwa shuleni alipokuwa akisoma, Shule ya Msingi Oysterbay jijini Dar, siku ya Ijumaa na mtu aliyejitambulisha kama shangazi yake na kutokomea naye kusipojulikana mpaka leo.
Akizungumza na Global TV, mama wa mtoto huyo anasema haelewi chochote tangu kupotea mtoto huyo na kinachomuuma amepotea katika mazingira ya shule ambayo yeye alikuwa anaamini ni salama kabisa kwa mwanaye.
Kama utamuona popote mtoto huyo wasiliana na mama yake kwa namba 0717 505 858