MTOTO ALIYEDAIWA KUSULUBIWA NA MAMA’KE… HALI NI MBAYA!

DAR ES SALAAM: Mtoto Hamisa Abduli (19), mkazi Kalokeni mkoani Mwanza, am­baye anadaiwa kuteswa na mama yake wa kufikia, hali yake ni mbaya ambapo amelazwa katika Hospitali ya Gamba mkoani humo.

 

Mtoto huyo anadaiwa kuteswa kwa muda mrefu na mama yake huyo ambapo kutokana na mateso hayo, mtoto huyo amedhoofu mwili huku akishindwa kutembea wala kuongea.

 

Akizungumza na kwa hisia kali, jirani ambaye alikuwa akishuhudia mateso makali aliyokuwa akiyapata mtoto huyo, alidai kuwa mara nyingi alikuwa akimuona akimpiga Hamisa ambaye anaumwa huku akimlazimi­sha atembee.

 

“Mimi ni mwanaume lakini mateso aliyokuwa akiyapata mtoto huyo ilinibidi tu nichukue hatua ya kuanza kujulisha vyombo vya habari ambapo nilianza kumtumia picha ya Hamisa, dada Flora (Lauo) ili aone hali ya mtoto huyo,” alidai jirani huyo.

Akiendelea kuzungumza kwa uchungu jirani huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alidai kuwa hivi kar­ibuni, mama huyo alimuacha mtoto huyo akiwa mgonjwa ndani na aka­wachukua watoto wake ambao wa­nalingana na Hamisa wakaondoka kwenda Kayenza.

 

“Kwa kweli baada ya kuona hivyo niliumia sana jamani ukiangalia mtoto anaumwa hawezi hata kuinuka  huku huyo mama kaondoka na watoto wake kamuacha ndani akiwa mgonjwa na mtoto mdogo kabisa ndio amsaidie halafu huku akizuia kisitumike hata chombo chake chochote kwa ajili ya kupika au kufanya chochote,” alidai jirani huyo.

 

Ijumaa Wikienda lilizungumza na baba mkubwa wa mtoto huyo aitwaye Mustapha Abdul ambaye alidai, si kwamba hawakuwa wanapenda kukaa na mtoto wa marehemu kaka yao lakini mama huyo alikuwa anamzuia. Alidai kuwa alikuwa ana­waruhusu kumsalimia tu na hata taarifa ya kuumwa kwake walizipata mtoto akiwa ames­hazidiwa.

“Mimi nakwambia huyo mama alishatuchosha kwani kaka yan­gu alimuoa mama wa Hamisa, baadaye alifariki na kumuacha na baba yake ndipo alipoolewa mama huyo lakini baadaye kaka yangu alifariki pia na kumuacha mtoto huyo hapo nyumbani.

 

“Sasa huyu mama tuliingia kwenye ugomvi mkubwa sana kutokana na vitendo alivyokuwa anavifanya na kila tukimuomba mtoto tukae naye sisi anakataa kabisa, tukajitenga naye lakini tulipigiwa simu na mtu kutuam­bia Hamisa ni mgonjwa sana na nilivyomkuta mtoto wangu katika hali mbaya niliumia sana,” alidai baba mkubwa wa Hamisa.

Mtangazaji wa Kipindi cha Nitetee, Flora Lauo ambaye alitoa ushirikiano mkubwa kupatikana kwa habari hii alisema kuwa mtoto Hamisa, anapatiwa matibabu sasa hivi katika hospitali ya Gamba lakini walimtafuta mama huyo wa kambo na kumpata na kumpeleka polisi ila ameachiwa kwa dhamana.

Flora aliwaomba Watanzania wenye mioyo safi kumsaidia cho­chote Hamisa ili aweze kupata matibabu, nguo za kuvaa na ma­hitaji mengine kwa namba 0759 665555.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

 

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Loading...

Toa comment