The House of Favourite Newspapers

MAAJABU: Mtoto Aliyepandishwa Juu ya BATI, Asimulia Alivyomuita ‘YESU’ – Video

SIKU chache zilizopita mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Maziwa, jijini Mbeya mkoani Mbeya alipatwa na tukio la ajabu ambalo limekuwa ni kitendawili kisicho pata majibu.

 

Mwanafunzi huyo Happy Mwakabenga amesema aliamua asubuhi kujiandaa kwenda shule ambapo alianza kwa kupiga mswaki kinywa chake ilikuendelea na maandalizi mengine.

 

Amesema akiwa ameshika Jagi lenye maji pamoja na mswaki alijikuta akiwa juu ya paa la Bati ya nyumba yao akiwa bado amashikiria vitu vyake vya kufanyia usafi wa kinywa.

 

Happy amesema kutokana na hali hiyo alimwamba Mungu na kupiga mayowe ilikuweza kusaidiwa baada ya kupata ufahamu kuwa yupo juu ya paa la Bati la nyumba yao.

 

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.