The House of Favourite Newspapers

Mtoto Anayeishi kwa Kunywa Mafuta Apata Ahueni

0
Dkt. Sufiana Rwezaura akizungumza na wanahabari

DAR ES SALAAM: Mtoto ambaye amekuwa akiishi kwa kunywa mafuta ya kula na kula sukari, Shukrani Kipango, alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili amefanyiwa vipimo na kukutwa na tatizo la sikoseli pamoja na upungufu wa madini ya chuma ambayo yamesababishwa na kutokula  vyakula  vya vitamini ili kumsaidia kutengeneza damu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo daktari bingwa wa magonjwa ya damu na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Damu  katika hospitali hiyo, Sufiana Rwezaura amesema kuwa ugonjwa huo ameurithi kutoka kwa wazazi wote wawili.

Dkt. Rwezaura amebainisha kuwa tatizo la sikoseli husababisha chembechembe nyekundu za damu kuwa na upungufu wa oksijeni kwenye damu, anapopata maambukizi yoyote zinabadilika na kuwa katika umbo la duara (selimundu) na zinapokuwa katika umbo hilo mwili unaziharibu kwa haraka na kupelekea upungufu wa damu mara kwa mara.

Amesema kuwa chembechembe hizo zikiharibiwa kwa wingi zinatengeneza nyongo ambayo husambaa kwenye mwilini na kuleta rangi ya njano au nyeupe.

Aidha amesema kuwa tatizo la kuvimba kichwa na maumivu makali linatokana na  chembechembe nyekundu  zinapobadilika na kuwa katika umbo la  selimundu  haziwezi kupita katika mishipa midogo ya damu na kusababisha damu kushindwa kutembea kwenda upande wa pili na kuleta uvimbe mwilini.

Mama wa mtoto Shukuru, Mwanabibi Mtei

Naye mama wa mtoto Shukuru, Mwanabibi Mtei ameeleza namna ambavyo mwanaye ambavyo amekuwa akiteseka kwa maumivu  na kubadilika rangi ya ngozi.

Mtoto Shukuru

Aidha mama huyo amewashukuru madaktari wa Muhimbili, serikali na wizara ya afya kwa kumsaidia mwanaye ambaye sasa anaendelea vizuri bila kula mafuta wala sukari tena.

NA DENIS MTIMA | GPL

Daktari Afafanua Juu ya Mtoto Anayeishi kwa Kula Sukali na Mafuta

Leave A Reply