The House of Favourite Newspapers

Mtoto atibua ndoa ya Vanitha

Hamida Hassan

Ndoa ya staa wa Filamu Bongo, Vanitha Omary juzikati ilitibuka baada ya mtoto anayeitwa Evrah kufananishwa na mumewe Paul Mtenda baada ya wawili hao kupiga picha pamoja.

Chanzo kilieleza kuwa, Evrah amechezeshwa kwenye filamu iitwayo Hadi Lini, baada ya kupigwa picha akiwa na Paul, watu wakaanza kuwapongeza kwa kukuza wakidhani ni mtoto wao aitwaye Precious.

Kufanana huko kwa Evrah na Precious kulimfanya Vanitha ahisi mtoto huyo ni wa mumewe (yaani wa nje), jambo lililoibua msuguano kati yao.

Kuhusu sakata hilo, Vanitha alisema: “Nilishtuka, wanafanana sana, mpaka tulipoenda kwa wazazi wa Evrah ndiyo nikatulia.”

Comments are closed.