The House of Favourite Newspapers

Video: Wazazi wa Mtoto Mwenye Kipaji Wafunguka Mazito

0

Mhariri Mtendaji Saleh Ally (kushoto), akiwa na baba Itham na Itham mwenyewe wakiingia Jumba la Habari Tanzania Global Publishers.

ITHAM Mahfudh mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu ambaye ana uwezo wa kuhifadhi,  kueleza na kujibu mambo mbalimbali anayoulizwa, leo ametembelea ofisi za Global Publishers Ltd akiwa na wazazi wake.

…akimsalimia Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo.

Mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera na aliyekuwa amefuatana na baba na mama yake aliyekuwa amembeba mdogo wa kiume wa Itham, alionyesha umahiri wa ajabu mbele ya waandishi wa habari kwa kujibu maswali mbalimbali kwa usahihi yakiwemo ya kisiasa, kijamii na matukio mbalimbali  yanayotokea nchini na nchi za nje.

Itham amepata umaarufu  huo kupitia video yake iliyokuwa ikimuonyesha akitaja majina ya viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika na duniani, ikiwemo pia miji mikuu ya nchi mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyochukua kiasi cha nusu saa,  baba yake alisema kipaji cha mtoto wao kilianza kuonekana mara tu alipoanza kuongea.

…akifafanua jambo katika simu ya mhariri mtengaji Saleh Ally

…akiwa na Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo.

…akiwa ndani ya studio za Global Tv na Wazazi wake.

Mhariri mtendaji Saleh Ally akifatilia kwa umakini mtoto Itham akifafanua jambo.

Stori Na Salum Milongo Picha na Mussa Mateja.

ITAZAME VIDEO HAPA…

Leave A Reply