The House of Favourite Newspapers

Mtoto kukojoa kitandani

0

photolibrary_rm_photo_of_sad_girl_on_bedWiki hii kwenye safu yetu nitakuandikia tiba ya mtoto kukojoa kitandani, kitu kinachosumbua wazazi wengi.

Dawa tunazo majumbani, lakini hatujui jinsi ya kuzitumia. Leo nitakuonesha tiba tofauti zitakazosaidia kumaliza tatizo.

Mafuta ya mzaituni

Kama mwanao ana tatizo hilo, chukua mafuta haya yapashe kidogo kisha mlaze mwanao, umpake yakiwa na vuguvugu chini ya kitovu kisha umfanyie masaji.

Mdalasini

Hakikisha mwanao anatafuna mdalasini kwa siku hata mara moja, kama hawezi kuutafuna chukua unga wake, changanya na sukari kisha weka kwenye mkate wenye mafuta mpe mwanao.

Ni tiba nzuri ambayo inasaidia haraka tatizo hilo.

Matunda damu

Mpe mwanao glasi ya juisi ya matunda damu saa moja kabla ya kulala, tumia tiba hii kila siku angalau kwa wiki kadhaa.

Kama ataendelea, mpe nusu kikombe kwa siku mara tatu, iwe kama dozi ya vidonge.

Leave A Reply