Mtoto mlemavu amlilia JPM
Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’
Na Igenga Mtatiro, UWAZI
MARA: Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Maria Maiya Marwa (15) wa Kijiji cha Kemakorere, Kata ya Nyarero wilayani Tarime, Mara, amelia na kumuomba Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’ kumsaidia gharama za kumuwezesha kutibiwa saratani ya ngozi nchini India baada ya kushindakana hapa nchini.
Akizungumza na gazeti hili akiwa nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Albinism wa Wilaya, Joseph Sinda mjini Tarime alipofikia kwa muda alisema alishindwa kufanikiwa kupona hali yake hiyo licha ya kufikishwa katika Hospitali za Muhimbili na Ocean Road zilizopo jijini Dar es Salaam alisema:
Maria Maiya Marwa
“Ninamuomba rais wangu Magufuli anisaidie gharama za kuniwezesha kutibiwa tatizo langu hili la kansa ya ngozi India kwani wazazi wangu hawana uwezo maana ni maskini,’’ alisema Maria huku akibubujikwa na machozi.
Binti huyo alisema kuwa kabla ya kufikishwa katika hospitali hizo, awali alipatiwa matibabu yake hayo Hospitali ya Wilaya ya Tarime na ile ya Rufaa ya Musoma kwa nyakati tofauti.
‘’Taarifa kwamba tatizo langu ni kansa ya ngozi lilifahamika kutoka kwa madaktari wa Hospitali za Ocean Road na Muhimbili, ambapo nilianza kutibiwa Juni 9, mwaka huu baada ya kufikishwa hapo Januari 27, 2016,’’ alisema Maria huku akifuta machozi.
Alisema kuwa awali alikuwa akipatiwa matibabu ya kawaida na kwamba Julai 26, mwaka huu aliruhusiwa kurejea nyumbani kwao na madaktari wa Hospitali ya Ocean Road na kutakiwa kurejea kuendelea na matibabu tena hospitali hapo Novemba 7, mwaka huu.
‘’Hapa mnapopaona nilipofungwa bandeji pana kidonda kilichokula sikio langu la upande wa kulia na kinauma sana, shingoni kuna sehemu imevimba, niliambiwa kuwa ni kansa ya ngozi, niliambiwa na madaktari hao kuwa nirudi kuendelea na matibabu tena baada ya miezi mitatu yaani tangu Julai 26, hadi Novemba 7, mwaka huu, sidhani kama muda huo utafika kama sitasaidiwa na rais kwani ninateseka mno maana sili vizuri kutokana na maumivu,’’ alisema Maria.
Kwa upande wake baba yake mzazi, Maiya Marwa ambaye aliangua kilio akijutia uhali duni alionao na familia yake hiyo, alisema hana jinsi ya kumuokoa kwa matibabu kwani hana kipato na kuwaomba watu wenye uwezo wamsaidie mwanae huyo ili akatibiwe nchini India.
Kwa walioguswa na mateso ya Maria watume misaada yao kwa simu namba 0766 128 337.
Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I
PT 2- Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I
Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3, O.F.M Yanyaka Tukio Zima