The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Rais Afariki Baada ya Kung’atwa na Mbwa

barrow Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi.

Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia, Adama Barrow amefariki akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuumwa na mbwa.

Habibou Barrow alifariki Jumapili baada ya kukumbwa na mkasa huo katika  eneo la Manjai karibu na Mji mkuu Banjul ambapo mazishi yake tayari yashafanyika.

Rais Mteule, Barrow ambaye ana wake wawili na watoto wengine wanne, yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa kuwa rais wa Gambia siku ya Alhamisi.

Comments are closed.