The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Mtoto wa CDF Mabeyo Wachukuliwa kwa Maziko

MWILI  wa Nelson Mabeyo ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) nchini, Venance Mabeyo, aliyefariki katika ajali ya ndege leo iliyoanguka katika  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, umechukuliwa na helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya maziko.

Nelson ambaye alikuwa rubani wa ndege ya Kampuni ya Auric Air yenye namba 5H-AAM amepata ajali katika uwanja huo akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi na wote kwa pamoja wamefariki dunia papo hapo.

 

Miili ya wawili hao  ilihifadhiwa katika Zahanati ya Soronera ikisubiri taratibu zingine. Helikopta hiyo imetua saa 8.35 mchana ikiwa na watu wanne.

 

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdini Babu amesema helikopta hiyo imeelekezwa ichukue mwili mmoja wa mtoto huyo wa Mabeyo na mwili wa Orutu aliyekuwa naye utabaki kusubiri ndege nyingine itakayokwenda Serengeti ikiwa na wataalamu wa masuala ya anga kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.

 

Kiongozi wa msafara kutoka JWTZ, Meja Makimboka, amesema wataalam wa jeshi watafika wakati wowote kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

 

Rubani Nelson Venance Mabeyo alihitimu kozi ya Urubani Flyers Flight Academy, Florida, Marekani mwaka 2017.

Comments are closed.