The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Elon Musk Amshikati Baba Yake Mahakamani, Atangaza Kubadili Jina la Ukoo

0

 

Bilionea Elon Musk akiwa na mkewe pamoja na kijana wake wa kwanza Xavier Musk

MTOTO wa tajiri namba moja duniani Bilionea Elon Musk ametangaza kufungua keshi mahakamani ili kubadili jina la ukoo la Musk na badala yake atumie jina la Mama yake mzazi kama utambulisho wake.

 

Elon Musk ana jumla ya watoto saba (7) ambapo watoto watano kati yao amezaa na mwandishi wa vitabu raia wa Canada Justine Wilson ambaye watoto wake wawili kati ya watano ni mapacha ambao ni Xavier Musk na Griffin huku wengine watatu ni Kai, Saxon na Damian, hawa watatu wote wamezaliwa kwa msaada kwa kupandikizwa mbegu Maabara kwa mfumo wa teknolojia ya In Vitro Fertilisation (IVF).

Bilionea Elon Musk akiwa na familia yake

Xavier Musk (18) ambaye amefungua kesi hiyo katika Mahakama ya Santa Monica California mnamo Aprili 18 dhidi ya baba yake mzazi Elon Musk Bilionea namba moja duniani ameomba kubadili jina kutoka Xavier Musk na kuitwa jina la ukoo wa mama yake na atambulike kama Xavier Vivian Jenna Wilson.

 

Kijana huyo amesema hataki kutambulika wala kuhusika na ukoo wa Musk kwa namna, muonekano au njia yoyote ile.

 

 

Vijana hao watano wa Elon Musk wamekuwa si watu wa kuonekana au kufahamka sana mitandaoni licha ya kuwa baba yao ni tajiri mkubwa na maarufu duniani.

 

Hadi sasa haifahamiki sababu ni nini ya kijana huyo mkubwa kutaka kubadili jina na kuachana na ukoo wa Musk lakini pia taarifa zinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa hata Elon Musk mwenyewe alikuwa hajui dhamira na mawazo ya kijana huyo juu ya maamuzi aliyochukua dhidi yake.

 

 

Leave A Reply