The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Harmonize Azua Balaa Zito!

0

 

DUNIA ina mambo kama alivyowahi kuimba mwanamuziki Seleman Msindi ‘Afande Sele’ akishirikiana Lameck Ditto, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linakuletea kasheshe la utata wa mtoto aliyedaiwa kuwa ni wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ au ‘Harmo’, karibu!

 

MADAI YALIPOANZIA

Iko hivi, saga hili lilianzia mitandaoni ambapo ‘pages’ mbambali zilidai kuwa, Harmo amepata mtoto huyo kwa binti anayejulikana kwa jina la Nasra Suleiman.

 

BETHIDEI YAZIDI KUNOGESHA

Good news ni kwamba, mtoto huyo ametimiza mwaka mmoja hivi karibuni na hiyo pia ni sababu iliyofanya wapenda ubuyu kuzidi kuchafua hali ya hewa huko mitandaoni.

“Yaani mtoto Harmo mtupu, hebu angalia pua yake, midomo ndiyo kabisa,” aliandika mmbeya mmoja kwenye ukurasa wake wa udaku kwenye Instagram.

 

Wambeya hao walikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba, Harmo amekuwa kimya kuhusu ishu hiyo kwa sababu anajua ni ya ukweli na anahofia kutia neno asije akagombana na mchumba wake mzungu, Sarah Michelotti.

“Wewe unadhani Sarah akiona Harmo anamzungumzia mtoto huyo itakuwaje wakati yeye hajapata hata moto mmoja,” alihoji mmbeya mwingine.

 

 

WENGINE WAKATAA

Hata hivyo, licha ya watu wengi kuonesha picha za mtoto huyo na kueleza anafanana kwa kila kitu na Harmo, wapo baadhi ya watu walisema hawafanani.

Walisema, kinachoendelea mitandaoni ni propaganda ya kumchafua Harmo ili kumharibia kwa mchumba wake Sarah.

 

UTATA WAIBUKA

Wakati fujo hizo zikiendelea mitandaoni, kuna mdau mwingine alichukua moja ya mahojiano ya Harmo ambayo yanaaminika aliwahi kuyafanya huko nyuma kuhusu mtoto huyo ambapo aliweka wazi kuwa mtoto huyo ni wake na yupo tayari kumhudumia.

 

“Haya sasa kiko wapi mliokuwa mnasema Harmo hataki kumuongelea mtoto huyu wakati alishawahi kumkubali huko nyuma,” aliandika mdau huyo ambaye ana ushawishi kwenye mitandao ya kijamii.

 

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI

Katika uchunguzi wake, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA liliweza kung’amua kwamba mama wa mtoto huyo alikuwa ni mmoja wa ma-video vixien wa Harmo kwenye wimbo wake wa Happy Birthday.

 

Baadhi ya taarifa zilieleza kuwa, uhusiano wa wawili hao ulichipukia hapo na kwamba ulikuwa wa siri mpaka pale mtoto huyo alipozaliwa.

 

“Unajua Harmonize alikuwa anapenda sana hii kitu isijulikane kwa sababu ya Sarah, ingeleta shida na sasa sijui nani amevujisha hii siri,” kilisema chanzo.

 

Lakini hata hivyo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilijiridhisha kutoka kwa watu wa karibu na Harmo ambao waliweka wazi kuwa Harmo alimtumia Nasra kwenye video yake hiyo ya Wimbo wa Happy Birthday, lakini hakufanya naye lolote.

“Ilikuwa ni video tu na baada ya hapo kila mtu aliendelea na maisha yake,” alieleza mtu wa karibu na Harmo.

 

 

HUYU HAPA NASRA

Ili kuondoa utata huo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linaamini anayejua baba wa mtoto ni nani huwa ni mama wa mtoto hivyo lilimtafuta Nasra.

Alipopatikana, Nasra alikanusha vikali mno kuwa hajazaa na Harmo.

 

IJUMAA WIKIENDA: Habari dada, hongera kwa kukuza mtoto.

NASRA: Asante sana, naongea na nani?

IJUMAA WIKIENDA: Mimi ni mwandishi wa Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, nataka kujua hii habari inayosambaa kuhusiana na wewe kuzaa mtoto na Harmo ikoje hii?

 

NASRA: Ni sehemu gani ambayo nilisema nimezaa na Harmonize au ulishasikia nimesema?

IJUMAA WIKIENDA: Madai ni mazito huko mtandaoni na hujawahi kukanusha au kukubali ndiyo maana tukaona kama mama utakuwa na majibu mazuri.

NASRA: Hizo habari si za kweli, huyo ni mtoto wangu mimi na si wa mtu mwingine.

IJUMAA WIKIENDA: Kwa hiyo ana baba yake?

 

Nasra: Ndiyo na siyo huyo unayemsema (Harmo).

IJUMAA WIKIENDA: Lakini kwa nini sasa wakusingizie wewe?

NASRA: Wamejisikia tu huwezi kuwazuia.

IJUMAA WIKIENDA: Shukrani sana.

HARMO ANASEMAJE?

Gazeti hili lilijaribu kumtafuta Harmo kwa njia ya simu, ilishindikana kumpata kwani simu iliita tu na hata alipotumiwa ujumbe hakujibu.

TUJIKUMBUSHE

Harmo amekuwa na misimamo pindi anapokuwa kwenye uhusiano. Alifanya hivyo alipokuwa na mwigizaji Jacqueline Wolper na sasa yupo kwa Sarah.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply