The House of Favourite Newspapers

Mtoto Wa Kiongozi Nguli Wa Dawa Za Kulevya El Chapo Asafirishwa Hadi Marekani

0

Mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya Joaquín “El Chapo” Guzmán amerejeshwa Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya, Mwanasheria Mkuu wa Marekani amesema.

Ovidio Guzmán anashukiwa kuongoza, pamoja na kaka yake, genge lenye nguvu la madawa ya kulevya la Sinaloa ambalo babake alianzisha.

Ovidio pia anadaiwa kuamuru kuuawa kwa mwimbaji ambaye alikataa kutumbuiza kwenye harusi yake.

Alikamatwa Januari katika jimbo la kaskazini mwa Mexico la Sinaloa na amekuwa kizuizini tangu wakati huo.

“Hatua hii ni ya hivi majuzi zaidi katika juhudi za Idara ya Sheria kushambulia shughuli za genge hilo,” Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland alisema katika taarifa yake kuhusu kurejeshwa nchini humo.

“Mapambano dhidi ya makundi hayo yamehusisha ujasiri wa ajabu wa watekelezaji sheria wa Marekani na watekelezaji sheria wa Mexico na wanajeshi, ambao wengi wao wamejitolea maisha yao katika kutafuta haki.”

Garland pia aliishukuru serikali ya Mexico kwa usaidizi wake katika kumpeleka Ovidio Marekani.

Hakukuwa na mwitikio wa haraka kwa uhamishaji huo na mamlaka ya Mexico.

Hatua hiyo inawadia siku chache baada ya mke wa babake mwenye umri wa miaka 33, Emma Coronel, kuachiliwa kutoka jela nchini Marekani baada ya kuhukumiwa mwezi Novemba 2021 kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Mumewe anatumikia kifungo cha maisha jela katika gereza la supermax huko Colorado kwa kuongoza genge la dawa za kulevya la Sinaloa.

Ovidio Guzmán ni mmoja wa watoto wanne ambao El Chapo alikuwa nao wakati wa uhusiano wake na Griselda López katika miaka ya 1980 na 90. Mkubwa zaidi kati yao, Edgar, aliuawa katika ufyatulianaji wa risasi mnamo 2008.

El Chapo pia ana watoto wengine kutoka kwa ndoa yake ya awali na kutoka kwa uhusiano wake uliofuata na Coronel.

RAIS SAMIA KWENYE ZIARA ya KIKAZI MTWARA, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KWENYE MKUTANONI…

Leave A Reply