Mtoto wa Lowassa Ajitosa Ubunge Monduli

MTOTO wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ni miongoni mwa wanachama watano wa CHADEMA waliochukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea ubunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.

Hii ni baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Julius Kalanga alijiuzulu na kujivua uanachama wa CHADEMA na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, amewataja wagombea wengine ni Cecilia Ndosi ambaye ni Mwenyekiti Baraza la Wanawake wa CHADEMA mkoa na Diwani viti maalum, Yona Laizer, Lobulu Kivuyo na Eric Ngwijo.

Aidha, amesema wagombea hao watapigiwa kura za maoni katika kikao kitakachofanyika kesho Jumamosi Kata ya Migungani wilaya ya Monduli.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment