The House of Favourite Newspapers

 Mtoto wa malkia hamjui Rihanna

WAKATI Rihanna akisumbua katika gemu la R&B na POP huku akishikilia tuzo 33 za Grammy, mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Prince Charles ameibuka na kusema kuwa hamfahamu.

 

Tukio hilo limetokea hivi karibuni ambapo Prince alikuwa na ziara ya siku 12 katika Visiwa vya Caribbean.

Wakati akiongea mbele ya wananchi, alisema Rihanna hamfahamu kabisa zaidi ya kuelezwa na mwanaye (Prince Harry) kabla ya kufika hapo.

 

“Simjui vizuri ila niliambiwa na mwanangu kuwa Rihanna amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki na ni nembo ya urembo duniani na kwa nchi hii…lakini pia atanieleza tena zaidi nimjue.”

Prince Harry na Rihanna walikutana mara ya kwanza 2016 alipotembelea katika visiwa hivyo katika kampeni maalum ya HIV/aids.

Comments are closed.