The House of Favourite Newspapers

Anusurika kifo kwa kuanguka kutoka ghorofani na kuchomwa na nondo

0

Mtoto anusutika kifo (3)

Mtoto Aman Vishwakarma akipatiwa matibabu.

Uttar Pradesh, India

MTOTO wa miaka 10, Aman Vishwakarma amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya nne hadi chini kisha kuchomwa na nondo huko Uttar Pradesh nchini India.

Mtoto anusutika kifo (5)Madaktari wakionesha kipande cha nondo walichokitoa kwenye mwili wa Aman Vishwakarma.

Inasemekana kuwa, Aman alipatwa na mkasa huo alipokuwa juu ya paa la ghorofa hiyo (ambapo ni nyumbani kwao) akifanya usafi ndipo akadondoka na kuchomwa na nondo yenye urefu wa futi nne, iliyozama kuanzia kwenye mgongo na ikatokeza kwenye makalio huku nondo hiyo ikikosa kidogo tu kuchoma kwenye uti wa mgongo wa mtoto huyo.

Mtoto anusutika kifo (1)Nondo ilivyozama kwenye mwili wa Aman Vishwakarma.

Aman anayetokea katika Wilaya ya Kaushambi mjini Uttar Pradesh nchini humo, amepona baada ya kufanyiwa upasuaji kwa saa nne na madaktari bingwa wa hospitali ya Narayan Swaroop waliofanya kila juhudi za kukitoa kipande hicho cha nondo na kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto huyo.

Mtoto anusutika kifo (6)Mama wa mtoto huyo, Kamla Devi (30) alizirai baada ya kuona hali ya mwanaye hospitalini hapo.

Mtoto anusutika kifo (4)Picha ya X-Ray.

Madaktari wamesema, ilikuwa kazi ngumu kwa kuwa nondo hiyo ilichana mshipa wake mkuu wa damu, kudhuru uti wa mgongo na mapafu pia hivyo kusababisha lita 2 za damu kuvujia kwenye tumbo la chakula.Mtoto anusutika kifo (2)

Leave A Reply