Mtoto wa miaka 14 Aibuka Kinara wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an
KIJANA wa miaka 14, Khamis Said ameibuka kinara kuhifadhi Qur- an kwa juzuu kumi katika mashindano madogo yaliofanyika leo Jumatatu kwenye msikiti wa Al Fattah, Keko Jijini huku mgeni rasmi akiwa ni alozi wa Iran, Ameer Mohammed Khan.
Katika mashindano hayo yalioshirikisha washiriki katika makundi sita ambapo ni kundi la juzuu moja, tatu, tano, kumi, 15 na 20 ambapo kijana huyo amefanikiwa kushinda na kupewa zawadi ya godoro la nchi 12 na pesa shilingi 160000, mshindi wa pili, Abduulkarim Bakari amepata godoro la nchi kumi na pesa shilingi 155000 huku mshindi wa tatu, Hindu Khamis akipata pia godoro la nchi 8 na pesa shilingi 150000.
Katika kundi la juzuu ya kwanza washindi ni Mariam Selema amepata zawadi ya dinner set ya PC 50 na glass, wapili Yassir Khamis (Dinner set 47) na watatu ni Rahma Juma (Hot Pot Pc 4), wengine katika kundi la juzuu ya tatu kwa upande wa wavulana ni Ibrahim Abdurahman (Godoro nchi kumi), Ausi Sadat (Godoro nchi nane) na Iddrisa Swalihina (Godoro nchi sita).
Kwa upande wa wasichana kwa juzuu tatu washindi ni Mwajuma Said (Godoro nchi nane), Zuwena Salum (Godoro nchi sita), Aisha Suleman (Dinner Set Pc 50). Washindi wa juzuu tano ni Suleiman Omary (Cherehani), Asma Mohammed (Godoro nchi 12) na Maliki Said (Godoro nchi nane). Washindi wa Juzuu kumi ni Asma Swaleh ( Godoro nchi kumi na pesa 140000), Hajra Twahir (Godoro nchi kumi na pes 130000) na Laila Ismail ( Chereheni na pesa shilingi 70000).
Washindi wa juzuu 15 ni Rehema Issa amepata godoro na pesa shilingi 155000, Ramadhani Iddy amepewa godoro na pesa shilingi 150000 na Ibrahim Said zawadi ya godoro na pesa shilingi 45.