Mtoto wa Miaka 4 aishi na maiti ya mama yake kwa siku 2

maittiBryan Allen akiwa na mama yake Shaleena Hamilton (enzi za uhai wake).maitinBryanmaitiiBaiskeli aliyozawadiwa Bryan.

BUFFALO, NEW YORK

POLISI mjiji Buffalo, New York nchini Marekani wamesema, mhudumu mmoja wa nyumba ya wageni mjini humo amemuokoa mtoto wa miaka minne, Bryan Allen aliyeishi ndani ya nyumba ya hiyo akiwa na maiti ya mama yake mzazi kwa muda wa siku mbili.

Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita huko Buffalo N.Y. Kwa mjibu wa vyanzo vya habari mjini Buffalo, mama huyo Shaleena Hamilton anasadikiwa kuwa alipatwa na mauti hayo ghafla wakati akiwa kwenye nyumba ya wageni alimokuwa amepanga. Uchunguzi unaonesha mama huyo alifariki kwa matatizo asilia

Taarifa zimeeleza kuwa mhudumu huyo, Taijuan Littleton awali alikuwa amepanga kuonana na Bi. Hamilton Desemba 4, akaenda moja kwa moja hadi kwenye nyumba hiyo iliyopo blok namba 1300, aligonga  mlango mara kadhaa bila kufunguliwa wala kuitikiwa, hivyo akaamua kumpigia simu japo na yenyewe haikupokelewa.

Kwenye kona kabisa ya mlango, Taijuan alisikia sauti ya mtoto akisema “hawezi kusikia, mama amelala.” Baadaye mtoto Bryan alifungua mlango baada ya kumwambia Littleton kuwa ameshindwa kumuamsha mama yake.

Alipokuta hali ile ndani mama yule mwenye umri wa miaka 43 akiwa amekufa tena mwili wake ukiwa sakafuni, Littleton aliamua kupiga simu polisi  na kumchukua Bryan kwenye gari lake la kazi, na kumfunika kwa blanket.

Polisi wanasema mtoto huyo alishindia maziwa na maple syrup kwa siku mbili ndani ya nyumba ile. Bryan kwa sasa yupo katika uangalizi wa ndugu zake.

Hata hivyo Polisi na wanafamilia wamempongeza Littleton kwa kumuokoa mtoto huyo na kumpatia Bryan zawadi ya baiskeli mpya na nyingine nyingi atapewa Jumatatu.

Loading...

Toa comment