Mtoto wa Mkulima Aliyefanya Maajabu Kidato cha 4, Div 1 ya 7 – Video

Yohana Lameck Lugedenga.

  MWANAFUNZI Yohana Lameck Lugedenga kutoka Shule ya Sekondari Igaganulwa iliyopo Kata ya Dutwa, Bariadi mkoani Simiyu, ambaye amepata division one ya pointi 7, katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2019, amefunguka mengi kuhusu maisha yake na wazazi wake pamoja na changamoto alizopitia wakati akisoma.

Yohana ambaye alikuwa akisoma katika shule hiyo ya kata amepata alama A katika masomo yote tisa, amekuwa akilelewa na mama yake mzazi huku baba yake akidaiwa kumtelekeza.

Katika mtihani wake wa kidato cha pili, FTNA 2017, Yohana alipata alama A katika masomo manane na moja akapiga B. Anasema alikuwa akisaidiwa na walimu kupata mahitaji yake kutokana na maisha duni ya nyumbani kwao.

Ufaulu wa mwanafunzi huyo umewashangaza wengi kutokana na mwanafunzi huyo kutokea katika familia duni yenye kipato cha chini na kudaiwa wakati mwingine kutohudhuria darasani kwa ajili ya kwenda kufanya vibarua ili aweze kumuhudumia mama yake Mariam Lulyalyana na bibi yake wanaomtegemea.

MWANAFUNZI Shujaa ALIYEONGOZA Nchi NZIMA Form 4, AONGEA kwa MARA ya Kwanza


Loading...

Toa comment