Mtu Mfupi wa Vituko Show Asifika kwa Mabongenyanya, (+ VIDEO Shilole alipoongea na wanafunzi).

Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA AMANI| MAKALA

DAR ES SALAAM: Bila shaka wewe ni mpenzi wa Program ya Vituko Show inayoruka hewani kupitia Televisheni ya Chanel Ten. Program hiyo hubebwa na wachekeshaji kibao   akiwemo Masele Chapombe, Asha Boko, King Majuto, Masai Nyota Mbofu, Man Dizo, Thabitha, Eric Kisauti, Kazi na wengine kibao.

Kazi Suleiman na baadhi ya wasanii wa vituko show

Wiki hii gazeti hili limefanya mahojiano mubashara na mmoja wa wachekeshaji hao aitwaye Kazi Suleiman almaarufu Kazi ambaye ukimuona unaweza kudhani ni mtoto kutokana na kuwa ‘mtu mfupi’ lakini ana umri wa miaka 36.

MAISHA YAKE HALISI YAKOJE?

“Mimi ni baba wa watoto watatu kwa wanawake wawili. Mmoja nilizaa naye watoto wawili. Mtoto wangu mkubwa ana umri wa miaka 16. “Kama ambavyo unajua mambo ya maisha, nikajikuta nimetengana naye. Baadaye nilikutana na mwanamke mwingine ambaye nimezaa naye mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu kwa sasa.

ALIANZAJE SANAA?

“Ilikuwa mwaka 1999. Wakati huo nilikuwa ninafanya kazi za ukondakta maeneo ya Mwenge (Dar). Hapo nilikutana na jamaa aitwaye Mrisho (naye ni mtu mfupi). Akaniambia anipe-leke kwa bosi wake, nikamk-ubalia, ndipo akanipeleka kwa jamaa aitwaye Khalfan ambaye ni bosi wa Al Riyami Productions (wazalishaji na wasambazaji wa kazi za sanaa).

ANAPENDA MWANAMKE WA AINA GANI?

“Kiukweli kabisa ninapenda wanawake mabongenyanya au matinginya ndiyo maana hata huyu niliyenaye kwa sasa ni bonge na ananizidi urefu.

“Sipendi mwanamke mfupi kwa sababu mimi ni mfupi, sasa tusije tukazaa mtoto mfupi kama chupa ya chai (anacheka kwa utani).

ALIKUTANAJE NA MCHUMBA’KE?

“Nakumbuka nilikuwa Mwanza kwenye shughuli zangu za sanaa. Nilimuona mwanamke mmoja akiwa anafanya biashara, nikavutiwa naye, nikamfuata na kuanza kuzungumza naye, akawa ananifahamu kwa sababu alikuwa anafuatilia kazi zangu. Hapo ndipo tukaanzia uhusiano wetu.

WAMEFUNGA NDOA?

“Hatujaoana na wala sijajitambulisha rasmi kwao ila Mungu akinijalia nitakamilisha kila kitu hivi karibuni kwani kila jambo lina wakati wake.

NI FILAMU GANI ALIZOFANYA?

“Nimefanya kazi nyingi sana ila ninazozikumbuka ni Mzee wa Bongo, Akakae Wapi, Rupia, Mimi Sikubali, Vioja, Bosi, Choo cha Kike, Mtaa wa Tatu na nyingine kibao.

JE, SANAA IMEMPA MAFANIKO GANI?

“Sijapata mafanikio makubwa kihivyo zaidi ya kufahamika na kupata fursa za hapa na pale, lakini sina nyumba wala gari ila naamini Mungu atanifanikisha tu kupitia kazi yangu ya sanaa.

JE, ANAKUTANA NA CHANGAMOTO ZA UMBILE LAKE?

“Najiona niko vizuri kabisa kama watu wengine na wapo ninaowazidi ila kuna watu wanahisi sisi watu wafupi hatuwezi kufanya vitu fulani, ndiyo maana kuna watu wengine huwa wananiuliza kuwa niliwezaje kufanya jambo fulani wakati mimi ni mfupi?

JE, NI KWELI WANASAMBAZA KAZI ZAO WENYEWE?

“Ni kweli tumeamua kusambaza kazi zetu wenyewe kwa kuingia mtaani. Kwa sasa tuko Wilaya ya Kahama na msanii mwenzangu, Rose tunapiga kazi pamoja na kuangalia fursa za kufungua duka kwa ajili ya kazi zetu.

KIPI KINACHOWAFELISHA WANAFUNZI?Loading...

Toa comment