The House of Favourite Newspapers

Mtu na Shangazi Yake Wanyofolewa Vichwa, Matiti, Sehemu za Siri

WANAWAKE wawili ambao ni mtu na shangazi yake, Kija Lushanga (70) na Pendo (40) ambaye jina la baba yake halikufahamika mara moja wamekutwa wamefariki dunia huku viungo mbalimbali vya miili yao ikiwemo kichwa, viganja vya mikono, sehemu za siri, na matiti vikiwa vimeondolewa.

 

Tukio hilo limetokea leo Jumamosi, Septemba 22, 2018 majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kijiji cha Lubanga, Tarafa ya Kasamwa, Wilayani Geita baada ya wanawake hao wanaosadikiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana kushambuliwa kwa mapanga.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio na kukuta kiganja kimoja kikiwa kimesahaulika na hadi sasa linawashikilia watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na mauaji hayo.

Comments are closed.