The House of Favourite Newspapers
  • Likes
  • Followers
  • Subscribers
  • Followers

Publisher Publisher - The House of Favourite Newspapers

  • Home
  • Habari
    • Kimataifa
    • Kitaifa
  • Global TV
  • Magazeti
    • Amani
    • Championi
    • Spoti Xtra
    • Ijumaa
    • Risasi
    • Uwazi
  • Ajira
  • Burudani
    • Audio Music
    • Music Videos
    • Photos
    • Dar Live
  • Michezo
  • Makala
    • Afya
    • Mahaba & Maisha
    • Burudani
    • Mikasa
    • Siasa
  • Tangaza
  • Hadithi
  • College
  • About us
Global Publishers
  • Home
  • Habari
  • Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi
gunners X
HabariKimataifa

Mtuhumiwa wa Mauaji Azidiwa Kizimbani, Jaji Aahirisha Kesi

On Jan 15, 2022
0
Share

Kesi ya mauaji inayomkabili Timothy Gitonga mwenye umri wa miaka 30, anayetuhumiwa kumuua bibi yake, Journes Kiringa mwenye umri wa miaka 80, imeshindwa kusikilizwa kufuatia mtuhumiwa huyo kuzidiwa na maradhi akiwa kizimbani.

 

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Embu, nchini Kenya ambapo mtuhumiwa alipoingizwa mahakamani, alianza kulalamikia maumivu makali aliyokuwa akiyahisi, jaji akaamuru kesi iendelee lakini mtuhumiwa aliendelea kulalamikia maumivu makali huku akionesha kuzidiwa.

 

Kufuatia hali hiyo, Jaji Tony Kwambai aliamua kusitisha usikilizwaji wa kesi hiyo na kuagiza mtuhumiwa apelekwe katika Hospitali ya Embu na baada ya matibabu arejeshwe katika Kituo cha Polisi Itabua kisha apelekwe tena mahakamani hapo ifikapo Januari 17, mwaka huu.

 

Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kudaiwa kumshambulia bibi yake na kumuua huku akimjeruhi vibaya babu yake, Jamleck Wamai ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Embu.

 

Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Rungana, Nembure ambapo sababu za tukio hilo hazijafahamika na baada ya kutenda ukatili huo, mtuhumiwa alitoroka kabla ya kukamatwa na polisi.

Related

BIMA PAP
Timothy Gitonga
0
Share
Global Publishers

Prev Post

Wanafunzi 10 Bora Kidato cha Nne

Next Post

Mbeya City Wanahitaji Sare tu kwa Simba

You might also like More from author
Habari

Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Afungua Mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi Tanga –…

Ajira

Usikose! Ajira 514 Zatangazwa Afya, TEHAMA na Ufundi – Deadline Disemba 23

Habari

Elon Musk Atambulisha XChat – App Mpya ya Faragha na Ukomo wa Mazungumzo

Habari

Waziri Mkuu Nchemba Awali Songea Kushiriki Ibada ya Heshima za Mwisho Jenista Mhagama…

Prev Next
Leave A Reply
Cancel Reply

You must be logged in to post a comment.



dstv
dstv
dstv


dstv


© 2025 - Global Publishers. All Rights Reserved.
Website Design: Yatosha Web Services
  • Likes
  • Followers
  • Subscribers
  • Followers