The House of Favourite Newspapers

Mtulia Rasmia CCM, Awajibu Wanaomtuhumu Kusaliti Upinzani

0
Mtulia wakati wa kukabidhiwa kadi ya CCM.

ALIYEKUWA Mbunge wa Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia leo Jumatatu Desemba 4, 2017 amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mapema leo katika ofisi za chama hicho.

YALIYOSEMWA NA MAULID MTULIA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA KADI YA CCM LEO

“Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli.

“Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee. Nimejiunga na CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli. Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli. Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi,” alisema Mtulia.

Akiapa wakati wa kukabidhiwa kadi hiyo.

“Sijaja CCM kutafuta cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote kile ninachokitaka. Kila jambo nililokuwa namwomba Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa) ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa.

“Nawashangaa Viongozi wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali na shughuli za Bunge, hizo shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo wanawasusia wenye mamlaka? Nipo tayari kuwa hata Balozi wa nyumba kumi na ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani Rufiji.

Hafla kumkabidhi kadi ikiendelea.

“Nawahaidi wana CCM watafurahia uwepo wangu na watanufaika nami ndani ya CCM. Nawaambia wana Kinondoni wasikosee, wachague Mbunge anayetokana na CCM. Wachague CCM siku zote,”  alisema Mtulia

IMETOLEWA NA;

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa.

 

CUF ya Lipumba Yamlipua Mtulia, Yaanika Figisu Zake Kabla ya Kuhamia CCM

Leave A Reply