The House of Favourite Newspapers

Mtunza Bustani Arusha Ajinyakulia Gari kutoka TBL

Promosheni ikichezeshwa kweye  droo inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga”.

 

 

KAMPUNI ya TBL leo imemtangaza mshindi mwisho ambaye ni wa tatu wa zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI, Gerge Isaya, ambaye ni  mtunza bustani katika Mkoa wa Arusha baada ya kuchezeshwa droo kweye promosheni inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga”.

 

TBL ilizindua promosheni hiyo inayojulikana kama ‘TBL kumenoga,Tukutane baa’ kwa lengo la kuwashukuru wateja wake na ilikuwa inafanyika kwenye baa mbalimbali nchini  ambapo washiriki waliweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya gari aina ya Renault KWDI kwa kila mshindi wa droo kubwa ya kila  mwezi.

 

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja TBL, David Tarimo, amesema promosheni hiyo ilikuwa ikifanyika kupitia chapa maarufu za bia zinazozalishwa na kampuni ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 

Aidha Tarimo ameeleza kuwa kampuni ya TBL itaendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuwapatia kile wanachokitaka na promosheni mbalimbali zitaendelea.

 

 

Comments are closed.