Mtupiaji Namba Moja Bongo Aingia Rada za Yanga

ADAM Adam, staa anayekipiga ndani ya JKT Tanzania anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambao wanahitaji saini yake. Nyota huyo ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilicholazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tunisia alipata nafasi ya kucheza pia kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya John Bocco ambaye alianza kikosi cha kwanza.

 

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Adam anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat trick alifanya hivyo Uwanja wa Mwadui Complex wakati, JKT Tanzania ikishinda mabao 6-1.

 

Kwenye orodha ya wafungaji anashika namba moja kwa wazawa akiwa amefunga mabao 6 sawa na raia wa Zimbabwe, Prince Dube wa Azam FC. Akizungumza kuhusu hilo, Adam amesema kuwa anazo ofa mkononi kwa sasa ila ataziweka wazi mambo yakiwa sawa.

 

“Ofa zipo za ndani na nje ila kwa sasa siwezi kuweka wazi mambo yapoje nikitulia nitajua na nitaweka mipango wazi,” amesema.

Chanzo: Spoti Xtra.

Toa comment